NA SAIDA ISSA, DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo, ameongoza matembezi ya hiari pamoja na zoezi la upandaji miti ikiwa na lengo la kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa ya kijani kuelekea siku ya Mazingira Duniani.
Matembezi hayo yamefanyika jijini Dodoma kutoka viwanja vya Bunge kuelekea eneo la Medeli ambapo shughuli ya upandaji miti imefanyika.
“Lazima tulinde nchi yetu maeneo mengi leo hii, yamegeuka kuwa jangwa ,mji huu ulikuwa hali yake mbaya sana siku za nyuma, lakini sasa hivi ukitoka juu kwenye ndege unaona Dodoma ilivyo ya kijani,
“Kigoma hoteli zimeshaanza kuvamiwa na Maji na wataalam wametwambia maji yameongezeka mita mbili, Leo hii ukiendaa baadhi ya nchi utaona mazingira yalivyoharibika kutokana na uchafuzi wa mazingira”alisema Jafo.
Jafo alisema kuwa hii ni siku maalumu kwajili ya upandaji wa miti, napia aliwashukuru waliokubali wito wa kukubali kuja katika siku hiyo ya upandaji miti.
“Na nikushukuru wewe muandaaji wa hii shughuli naona umeratibu vizuri haya matembezi hata wale wenye vitambi Leo wametembea na ninaimani kutembea leo colesto zimepungua”alisema Jafo
Pamoja na hayo Waziri Jafo, aliagiza kila halmashauri nchini kupanda miti milioni moja na laki tano, ambapo alisema wameazisha kampeni ya mazingira ili kila mtu aweze kuhusika.
Alisema kuwa kutakuwa na kampeni ya mazingira na hii nikutokana na miti milioni 48, kila mwaka inakatwa hivyo kampeni hiyo itashirikisha kila mtu na hii itakuja na mashindano ambayo itashindanisha, Mikoa Bora, halamashauri za wilaya, miji , kata na vijiji , vyuo, shule za msingi na sekondari na huku zawadi Kama magari zikitolewa kwa washindi.
“Tunataka Tanzania iwe ya mfano na kwenye taasisi za serikali tutapanda miti ya matunda, wakuu wa mikoa sasa tuhakikishe tunaenda kupanda miti katika maeneo yetu natamani kila mwanafunzi awe na miti mitatu na kuitunza jambo hili litakuwa jema Sana na suala hili lishuke hadi kwenye ngazi za familia” alisema.