LONDON, England
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema, Manchester City isingeshinda ubingwa wa England msimu huu ikiwa wangelikabiliwa na wachezaji wenye maumivu.
Beki wa kati wenye ushawishi, Virgil van Dijk na Joe Gomez walikosa msimu mwingi wakiwa na maumivu ya goti.
Mlinzi mwenzake, Joel Matip, viungo Fabinho na Jordan Henderson na mchezaji mpya aliyesajiliwa, Diogo Jota walikuwa miongoni mwa wale ambao pia walikosa sehemu kubwa za kampeni.
“Pamoja na maumivu yetu haukuwa mwaka wa kuwa mabingwa”, alisema, Klopp.
“Hakuna nafasi kwa mtu yeyote.
“Kama walivyo wazuri, ikiwa ManCity wana nusu ya mabeki wa kati wapo nje, hapana [hawatashinda ligi]. Mabeki watatu wa kati [Manchester] United, hapana.
“Tumepambana kidogo, tumekubali matatizo na tumefanikiwa, na ikiwa tutashinda Jumapili, na ikiwa tunafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi tumefanikiwa zaidi. Ndio hivyo.”
Licha ya kuwa juu ya msimamo wakati wa Krismasi, athari za maumivu ya wachezaji mwishowe zilikikumba kikosi cha Klopp.
Lakini walirudi njia ya mstari kwa ushindi wa mechi saba katika michezo tisa ikimaanisha kwamba ikiwa watashinda mechi yao ya mwisho nyumbani dhidi ya Crystal Palace watapaswa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati wa kampeni yao ya kushinda taji msimu uliopita Klopp mara nyingi aliwasifu wachezaji wake kama ‘wanyama wa akili’.
“Ni wazi tusingelikuja hali hii ikiwa wachezaji wasingelionyesha tabia ya aina hii. Wana tabia maalum”.
“Wachezaji walithibitisha sasa mamilioni ya nyakati, sio juu ya mawazo yao au tabia yao ikiwa kuna kitu kimekwenda vibaya.
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema, mabingwa hao wapya wa England, lazima wajifunze kutoka utetezi mgumu wa taji wa Liverpool mwaka huu na wasichukulie kitu chochote poa msimu ujao.(Goal).