NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya (KMKM) itaendelea kufanya vyema ili kutwaa taji la ligi kuu Zanzibar na kuiwakilisha Zanzibar kwenye michezo ya kimataifa.
Makame Mshenga Makame ni afisa habari wa timu hiyo aliyasema hayo huko Maisara alipokuwa akizungumza na gazeti hili, juu ya mikakati ya kumalizia michezo ya ligi kuu Zanzibar.
Alisema kati ya hizo wanatarajia kuanza na KVZ Mei 22 ambapo wanatarajia kucheza uwanja wa Amaan.
Hivyo aliwataka wadau na wapenzi wa KMKM kuwaunga mkono katika mechi zao,ili kufikia malengo yao,huku wakiamini kuwa msimu huu ubingwa utakuwa wao.
KMKM inaongoza ligi ikiwa na pointi 36 ambapo mwaka 2019-2020 ilifanikiwa kuchukua ubingwa 2020-2021 ulichukuliwa na Mlandege.