NA NASRA MANZI

JUMUIYA ya Madaktari wa Kichina Zanzibar (China medical Team) wamesema wataendelea kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwapatia huduma za afya wananchi wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara maalum iliyofanywa na madaktari hao katika hospitali ya Mkoa Kaskazini iliyopo Kivunge, mmoja wa madaktari hao Wang Yiming alisema watatekeleza vyema majukumu yao endapo watapata ushirikiano.

Alisema timu ya madakatari wa China waliopo Zanzibar wapo tayari kwa wakati wote kushiriana na serikali sambamba na kubadilisha mawazo na mataalamu wa afya wazalendo.

Dk. Yiming alisema mahusiano yaliopo kati ya Zanzibar na China yamesaidia kwa kiasi kikibwa kuwepo manufaa mengi yakiwemo ya kiafya.

Pia alisema huduma hizo kwa wananchi kutawaondoshea usumbufu wa maradhi yanayowakabili ili kusudi kupunguza wimbi la maradhi.

Yiming alisema lengo la kubwa kutoa huduma bora kwa wanajamii pamoja na kuisaidia serikali katika sekta ya afya kwa kupata matibabu bila ya malipo.

‘’Kwa sasa timu ya madaktari wa kichina tumekuwa kukiendelea kubadilishana utaalamu wa teknologia na madaktari wa hapa hii inatupa faraja ya kuimarisha huduma kwa wanajamii’’, alisema.

Aliongeza kuwa magonjwa ya koo, maskio, meno na maradhi ya wanawake ni moja ya maradhi yaliyoiandama sehemu kubwa ya jamii hapa Zanzibar.

Nae Daktari dhamana wa hospitali ya Kivunge, Tamim Hamad alisema licha ya matibabu yaliyotolewa na waatalamu hao bado madaktari wananufaika kwa kupatiwa mafunzo na ushauri wa mara kwa mara kutoka kwa timu hiyo.

Aidha daktari Tamim akizungumzia maradhi yanayowasumbua wananchi wa kaskazini kuwa ni pamoja na kisukari na presha.

Kwa upande wa wananchi walisema wamefarajika kupata huduma hizo kwa wananchi mbali mbali Sambamba na kuitaka jumuiya hiyo ya kichina kuendelea na utaratibu wa kuchunguza Afya zao kila mara.