RIO DE JANEIRO, BRAZIL

WATU wasiopungua 25 wameuawa na wengine watano walijeruhiwa katika mapigano makali huko Kaskazini mwa Rio de Janeiro kati ya polisi na watuhumiwa wa walanguzi wa dawa za kulevya.

Kulingana na Polisi wa Kiraia wa Rio de Janeiro, afisa mmoja wa polisi alikufa kutokana na kupigwa risasi, wakati watu wengine 24 waliouawa walidaiwa kuwa ni walanguzi wa dawa za kulivyo na makundi ya kihalifu la ‘Favela’ la Jacarezinho.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya asubuhi huko Jacarezinho wakati wa operesheni ya Polisi dhidi ya biashara ya dawa za kulevya na uhalifu katika eneo hilo.

Hata hivyo, kulikuwa na rikodi za sauti ya video kwenye mitandao ya kijamii vilionyesha mapigano makali ya bunduki na milipuko ya bomu ya gesi katika sehemu kadhaa za favela, na picha zilizochukuliwa kutoka kwenye helikopta zilionyesha watu wenye silaha wakikimbia huku na kule.

Jacarezinho inaongozwa na kile kinachoitwa Amri Nyekundu, kikundi kikubwa zaidi cha uhalifu huko Rio de Janeiro.

Tofauti na makazi duni mengi ya jiji ambayo hukaa kwenye milima, Jacarezinho iko katika eneo tambarare ambalo wahalifu wameweka vizuizi ili kufanya iwe vingumu kwa vikosi vya usalama kufikia.

Amri Nyekundu inadaiwa kufanya mauaji kadhaa, wizi, visa vya utekaji nyara na kuajiri watoto kwa biashara ya dawa za kulevya huko Jacarezinho.