VATICAN, ITALIA
KIONGOZi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ametoa wito wa kukomeshwa ghasia katika eneo la walowezi la mashariki mwa Jerusalem, ambako mapigano kati ya Wapalestina na polisi ya Israel yamesababisha idadi kubwa ya wapalestina kujeruhiwa.
Baada ya kuongoza ibada ya Jumapili katika kanisa la mtakatifu Petro la mjini Vatican, Papa alisema amekuwa akifutailia kwa hali ya wasiwasi mkubwa yale yanayotekea Jerusalem.
Katika wito wake huo ametaka ushiriki wa kila kundi katika kuleta suluhisho la mzozo huo kwa shabaha ya kurejesha heshima ya mji huo mtakatifu ili mahusiano mema yaweze kutawala, akisema vurugu zinaongeza vurugu.
Hali ya mvutano imeongezeka leo hii huko mashariki mwa Jerusalem baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa mwishoni mwa juma kulikotokana na mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya Israeli, na kusababisha hofu kwa ulimwenga kwamba machafuko hayo yanaweza kusambaa zaidi.