NA MWANAJUMA MMANGA

JUMUIYA ya wazee Zanzibar (JUWAZA 11) imetoa msaada  wa futari ya vyakula mbaIi mbali kwa wazee wasiojiweza, ili kupunguza makali  katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Msaada huo  wa  vyakula hivyo vilivyotolewa ni pamoja na mchele, Unga wa Ngano, Mafuta ya kupikia na tende kwa watu 100.

Akikabidhi msaada huo wa futari  kwa wazee, Msaidizi wa Rais mambo ya siasa, Ali Salum Haji (kirova),  aliyasema hayo huko ofisi za jumuiya hiyo Mikunguni Mjini Unguja.

Kirova, alisema msaada huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, baada ya jumuiya hiyo kufika ofisini kwake Ikulu kuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ya jumuiya yao ikiwemo ukosefu wa ofisi pamoja na masuala mengine.

Alisema taasisi hiyo imesajiliwa kihalalli na kikubwa hivi sasa inasimamia wazee wengi na wanahitaji huduma nzuri na zilizobora ambazo zitawasaidia hasa wale wasiojiweza.

“Wazee ni klila kitu bila ya wazee hakuwezi kupatikana ushauri mzuri mbao utaweza kuleta matunda, hivyo ni vyema jumuiya hii kuwa na waangalifu katika kuwajali na kuwasimamia wazee hao”alisema.

Aliongeza kusema kuwa Rais alisistiza zaidi aliitaka jumuiya hiyo kufanya biashara ya kanga  ambazo za kuonba kura ya Rais Dk Hussein Mwinyi ili kuweza kujikimu katika kuendelza jumuiya hiyo.

Alisema lakini pia taasisi hiyo itaweza kusimama imara kupitia biashara hiyo wakiuza itakuwa endelevu kwani wataweza kupunguza changamoto mbali mbali zitaweza kutatua kwa haraka.

Alisema Dk. Hussein Mwinyi aliwataka watu wenye uweo kuelekeza zaidi kuwasaidia watu wasiojiweza ili kuishi kama watu wengine sambamba na kupata fadhila kwa mtume muhammda salawahu Alayhi Wassalam.

Nae Katibu wa Jumuiya hiyo Katibu wa Jumuiya hiyo, Amani Suleiman, amesema wanashukuru kupokea msaada huo kwa Rais Dk, Huseein Mwinyi na mungu atamlipa ujira wake

Kwa upande wao wazee hao wameskuru kupata msaada huo kwani muda muwafaka, hivyo amewaomba watu wengi wenye uwezo na taasisi kuwasadia wazee ili kupata fadhila za Allah Subhanahu wataala kama alivyoamrisha bwana mtume.

Sadaka hizo zimetolewa katika maeneo mbali mbali ikiwemo mashamba na mjini na Rais Dk, Hussein Mwinyi  ili kupunguza makali ya hali ya saumu.