LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha timu ya Taifa ya England na Manchester United, Marcus Rashford, ametunukiwa nishani ya heshima ya kuwa sehemu ya Ufalme wa Uingereza (MBE).

Hii ni kutokana na namna  alivyopambana kuhakikisha serikali inabadili sera zake kwa Wanafunzi kupata chakula bure skuli, lakini pia harakati zake za kutoa michango na misaada mingine ya kijamii kwa Watoto nchini Uingereza.

Heshima hii kwa kawaida hutolewa kwenye kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya Malkia Elizabeth.