NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Simba Meddie Kagere, amesema pamoja na kukosa nafasi kwenye kikosi chake cha Simba lakini anaangalia zaidi matokeo mazuri.
Hivi karibuni Simba ilitolewa kwenye michuano ya robo fainali na timu ya Keizer Chiefs FC ya nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na Zanzibar Leo Kagere alisema kwamba ni kweli anakosa nafasi lakini jambo hilo halimpe shida.
Alisema kikubwa ni kuwaombea dua wanaopangwa kupata ushindi ili hata kama kuna bonasi zinatolewa ziweze kupatikana na kuwasaidia katika maisha lakini pia kufanya vizuri ndio malengo ya kila timu.
Alisema hawezi kuwaombea wenzake waliopangwa wafanye vibaya eti kwa sababu yeye sio sehemu ya kikosi kitu ambacho sio cha kibinaadamu.