NA MWANAJUMA ABDI, DAR ES SALAAM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo anatarajia kufanya mkutano na zaidi ya wazee 900 wa mkoa wa Dar es Salaam, ambao watajadili masuala mbali mbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amesema kikao hicho kitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

Aidha ametoa wito kwa wazee waliopata mialiko ya kushiriki katika kikao hicho kujitokeza kwa wingi ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia amewaitia.

Kwa upande wao viongozi wa wazee wamemshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kukutana na wazee huku wakisema wanatarajia kikao hicho kitakuwa na manufaa makubwa kwao.