Yatoa maagizo mazito kwa Wizara,TFF
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuhakikisha wanataja tarehe mpya ya mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga haraka iwezekanavyo.
Hatua hiyo inafuatia mchezo huo wa marudiano wa ligi kuu Tanzania Bara kutofanyika Jumamosi ya Mei 8 baada ya kutokea mkanganyiko wa muda wa kuanza hatimaye kuahirishwa.
Pamoja na hayo, Waziri Mkuu Majaliwa akizungumza Bungeni Jijini Dodoma jana pia ameagiza Wizara hiyo na TFF kushughulikia hatima ya mashabiki waliolipa viingilio kwa ajili ya mchezo huo.
“Tumeiagiza Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa kuhakikisha kwamba wanatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania mchezo wenyewe utachezwa lini, lakini pia vile viingilio vya Watanzania waliokuwa wamenunua (tiketi) kuingia kwenye mchezo ule hatima yake ni nini,”.
Waziri Mkuu, amewasihi Watanzania kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo.
Tangu kutokea kadhia hiyo tayari TFF nayo imetoa tamko lake pamoja na klabu Simba, ambazo zote zimeelelezea kadhia hiyo.
Gomez alisema maandalizi yote ya mchezo yalikamilika na wachezaji walikuwa tayari kuelekea mchezo huo lakini hakuna namna kwani imeshatokea.
Raia huyo wa Ufaransa ameongeza kuwa alipenda kukutana na Yanga kabla ya kucheza mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chief ili kuongeza utimamu kwa wachezaji lakini imeshindikana hivyo tunajipanga kwa mechi ijayo.
“Wachezaji walikuwa tayari kwa ajili ya mchezo huu na maandalizi yalikuwa yamekamilika. Tulitamani tucheze mechi ya leo ili kuongeza utimamu kwa wachezaji lakini imeshindikana hivyo tunajiandaa kwa mchezo ujao,” amesema Kocha Gomez.
Kocha mkuu wa timu ya Simba Didier Gomez alisema anaamini mkanganyiko uliotokea utamalizwa baada ya pande zote kukutana na kuzungumza huku akiwapa pole mashabiki waliojitokeza kwa wingi kutaka kushuhudia mtanange huo ambao haukufanyika.
Raia huyo wa Ufaransa aliongeza kuwa alipenda kukutana na Yanga kabla ya kucheza mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chief ili kuongeza utimamu kwa wachezaji lakini imeshindikana hivyo tunajipanga kwa mechi ijayo.
Afisa habari ya Simba Haji Manara alisema hana nia ya kulaumu kwa kuhairishwa mchezo huo, lakini ameumizwa sana kuona mashabiki wake hawakupata walichokitarajia.
Kwa sasa TFF wameeleza kuwa wanalifanyia kazi suala hilo ili kujua hatma ya mchezo huo ambao umesababisha hasara kubwa na inakuwa ni rekodi ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kutokea.