TEL AVIV, ISRAEL

SHAMBULIZI la risasi katika gari moja iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi katika Ukingo wa Magharibi majira ya jioni hapo juzi lilijeruhi Waisraeli watatu, kati ya hao wawili wako katika hali mbaya, viongozi wa Israeli walisema.

Msemaji wa jeshi la Israeli alisema katika taarifa kwamba “gari linaloshukiwa” liliwasili katika eneo la Tapuah, nje ya makazi ya Wayahudi ya Tapuah, na kuwafyatulia risasi Waisraeli ambao walikuwa wakingojea usafiri katika kituo cha basi.

Hata hivyo, taarifa zilisema kuwa vikosi vya usalama vilijibu sahambulizi hilo ikiwa ni pamoja na kuliteketeza kwa moto gari linaloshukiwa wakati likitaka kutoroka gari hilo.

Kitengo cha huduma ya afya ya dharura cha Magen David Adom kilisema katika taarifa kwamba watu wawili walijeruhiwa vibaya na mwingine alijeruhiwa kidogo, watu hao watatu walihamishwa katika hospitali nchini Israeli.

Vikosi vya usalama vya Israeli vilianzisha msako wa kuwapata wahusika. “Askari katika eneo hili walizuia njia kadhaa na kwa sasa wanatafuta utaratibu wa kisheria na kuwatia nguvuni wahusika.