NA VICTORIA GODFREY
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu wa mguu mmoja na mkono mmoja Zanzibar, limesema lipo mbioni kukamilisha rasimu ya katiba.
Kwa sasa wanafanya kazi zao chini ya Chama cha Michezo kwa watu wenye Ulemavu Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili rais wa Shirikisho hilo Hassan Haji Silima, alisema mchakato wa rasimu ya katiba unaendelea hadi sasa kupata usajili rasmi wa Shirikisho hilo.
Alisema wanatarajia kupata hati ya usajili hivi karibuni ili kutambuliwa rasmi.
“Tupo kwenye rasimu ya katiba mpaka muda huu tunatarajia mpaka mwezi huu kupatiwa hati ya usajili na sasa hivi tupo katika Chama cha Michezo kwa Watu kwenye Ulemavu Zanzibar .