MOGADISHU, SOMALIA
VIONGOZI wa kisiasa nchini Somalia amefikia makubaliano ya pamoja kwa kutaka nchi hiyo iandae uchaguzi mkuu utakaotoa viongozi wa mpya katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Somalia iliingia kwenye mzozo mkubwa wa kisiasa kfuatia nchi hiyo kushidwa kuandaa uchaguzi mnamo mwezi Februari mwaka huu na bunge kuchukua hatua ya kumuongezea kubakia madarakani rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo.
Mikutano ya kusaka suluhu ya kisiasa nchini Somalia ilisimamiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo, Mohamed Hussein Roble ambapo aliwakutanisha viongozi wa majimbo na wakisiasa kuuondoa mkwamo uliopo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Hussein Roble, alisema hatimaye suluhu imepatikana na kwamba nchi hiyo iandae uchaguzi mkuu.
“Hatimaye suluhu imepatikana, kilichoamuliwa na viongozi wa majimbo na wa kisiasa ni kundaliwa kwa uchagu mkuu mpya utakao kuwa huru na wa haki”, alisema.
Mkwamo wa kisiasa nchini Somalia tayari ulikwisha anza kuleta hofu dhidi ya kundi la kigaidi nchini humo la Al Shaabab kupata nguvu tena za kufanya hujuma.
Hata hivyo bado haijafahamika tarehe rasmi ambapo nchi hiyo itaandaa uchaguzi.