NA VICTORIA GODFREY
TIMU ya Tambaza Youth imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Boom katika mashindano ya Jiandae Cup wilaya ya Ilala uliochezwa juzi kwenye dimba la Airwing,Dar es Salaam.
Dakika ya 21 Devis Emmanuel wa Tambaza alifunga bao la kwanza na Salim Ndodi aliongeza la pili dakika ya 32, Boom ilipata bao la kufutia machozi kipindi cha lala salama kupitia Khalid Khalid dakika ya 89.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA) Daud Kanuti, alisema mashindano yanakwenda vizuri na ushindani mkubwa.
Alisema timu zote zimecheza vizuri kila mmoja apate matokeo mazuri na hilo limewezekanana kupata mshindi wa mchezo huo.
” Niwapongeze timu zote mbili kwa kuonyesha mchezo mzuri na wa ushindani kwani tunaimani malengo yetu yatatimia kwa timu kuwa imara katika ligi zijazo.
Alisema malengo ni kuwaandaa wachezaji na makocha kupata nafasi ya kubaini kasoro ambazo watazifanyia kazi waonyeshe ushindani katika ligi daraja la Tatu na Nne .