NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA

TANZANIA na Kenya zimesaini makubaliano manne kati ya 64 ya kiuchumi katika nyanja za kibiashara ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa nchi hizo waliokutana jijini Nairobi , nchini Kenya Mei 4 na 5, mwaka huu, kujadili masuala mbalimbali yanayokwaza kibiashara.

Akiongea na vyombo vya habari jiji Arusha mara baada ya kutiliana saini Makubaliano hayo katika Mkutano uliofanyika jijini Arusha,waziri  wa viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo alisema Kuwa makubaliano hayo ni miongoni mwa masuala 64 yaliyopo kwenye mchakato wa kufanyiwa kazi na nchi hizo.

“Tumekubaliana masuala makubwa manne ambapo bidhaa za Tanzania Kama vile vinywaji baridi vya juice vitaingia Kenya bila kikwazo , kuondolewa ada ya ukaguzi kwa bidhaa Kama unga wa ngano ambazo zitakuwa na nembo ya  ubora kutoka TBS ya Tanzania, kuwezesha upitishaji wa mshindi bila kikwazo na kuondoa ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za kioo kutoka Tanzania kwenye Kenya”alisema .

“Kwa kupande wa Kenya tumekubaliana kutoa upendeleo kwa bidhaa za simenti ,juice zinazozalishwa nchini kenya  zinazokidhi matakwa ya vigezo vya uasili ya bidhaa za jumuiya ya Afrika mashariki Kama Sheria ya forodha inavyosema na bidhaa zinazoharibika haraka Kama vile Maziwa zinapewa kipaumbele na kuongeza kibali Cha kuingiza mifugo kutoka siku 15 Hadi 30”

Aliongeza kuwa makubaliano mengine yaliyobaki yataendelea kufanyiwa kazi na wataalamu wakiwemo makatibu wakuu wa wizara  wa pande zote na baada ya miezi mitatu watakutana tena nchini Kenya kwa ajili ya kuendelea na Mkutano wa makubaliano.

Alifafanua Kwamba kati ya Makubaliano 64  masuala  30 yamepatiwa Suluhu na 34 yanaendelea kufanyiwa kazi na yapo katika hatua mbalimbali ya kukamilika .

Kwa upande wake waziri wa Maendeleo ya viwanda na biashara wa nchini Kenya , Betty Maina alisema Mkutano huo wa kwanza umekuwa na mafanikio makubwa ya kutatua changamoto zote zilizokuwa zinaibua wafanyabiashara .

Alisema makubaliano hayo ni Utekelezaji wa mawazo ya viongozi wakuu wa nchi, Rais Samia Suluhu wa Tanzania na Rais Kenya, Uhuru Kenyatta ambapo Mambo 30 yamepata Suluhu na mambo 34 yatapata Suluhu ndani ya miezi mitatu.

“Biashara Kati ya nchi ya Kenya na Tanzania ni kitu muhimu Sana tunataka soko la Tanzania na Kenya liwe kubwa na tunataka nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kupata kupatamasoko ya unakika “alisema Maina.

Mkutano huo wa siku tatu uliwashirikisha wataalamu mbalimbali,makatibu wakuu ,mawaziri kadhaa wa pande zote za nchi ya Kenya, Tanzania na Zanzibar.