NA VICTORIA GODFREY

TIMU 18 zimethibitisha kushiriki mashindano ya Kigamboni Super Cup ambayo yamepangwa kuanza Mei 15 kwenye viwanja mbalimbali wilayani Kigamboni.

Mashindano hayo yatachezwa kwenye viwanja vinne ambavyo ni  Dege,Mzima,Kibada na skuli ya msingi Kigamboni.

Akizungumza na gazeti hili Katibu wa  Mashindano wa Chama cha Soka Wilaya ya Kigamboni(KDFA) Issa Yahya’ Kiiza’ alisema maandalizi yamekamilika.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao na kupata wachezaji watakaounda timu ya wilaya hiyo kwa kujiandaa na mashindano au ligi  mbalimbali.

” Tumekuwa tukiendesha ligi, mashindano mbalimbali yakiwemo haya yatakayoanza hivi karibuni, kwa nia ya kuinua na kuendeleza soka wilayani hapa,hivyo maandalizi yapo vizuri na sasa tunasibiri timu tu,” alisema Kiiza.

Alizitaja timu hizo ni pamoja Magogoni, Kibada Rangers, Muungano, Gold Land, Navy,Tuamoyo,Dege.Madina,Mzima,ABC,Mkwajuni,Rungu,Red Sea,Kigamboni Soccer,Ungindoni African,Vijibweni na Amani City.