NA VICTORIA GODFREY

TIMU ya Tuamoyo imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya soka la Vijana chini ya umri wa miaka 20 katika hatua ya robo fainali.

Tuamoyo umepata nafasi hivyo baada ya kuiibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 dhidi ya Somangila  mchezo uliocheza kwenye Uwanja wa skuli ya ya Msingi Kigamboni, Dar es Salaam.

Dakika ya 20  Tuamoyo ilipata bao  lililofungwa  na Omary Said, kabla ya Salim Costa kuongeza mabao mawili dakika ya 30 kwa pelnati na 35 ,huku Somangila walipata bao dakika ya 25 lililofungwa Ausi Ndoka na la pili Joefrey dakika ya 80.

Kutokana ushindi huo Tuamoyo itaungana na Kigamboni Soccer, Kim Canteen na Kizito katika  hatua ya nusu fainali ambacho ni kinyang’anyiro ya kusaka timu itakayofuzu kwenda fainali.

Akizungumza na gazeti hili Katibu wa Kamati ya Mashindano wa Chama cha Soka Wilaya ya Kigamboni (KDFA) Issa Yahya ‘ Kiiza’ alizipongeza timu zilizoingia  hatua ya nusu fainali na kuzitaka zikajipange ili waweze kutoa burudani hatua ya nusu fainali.

” Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua tuliyofikia maana tulianza na timu nyingi na sasa tumebakiwa na nne ambazo zitacheza nusu fainali, tuzikumbushe bado safari ipo vyema kwenda kujipanga ,” alisema Kiiza.

Aliongeza baada ya kumalizika kwa ligi watachagua wachezaji watakaounda kombaini ambayo itaandaliwa kwa mashindano mbalimbali yajayo sambamba na kulinda vipaji na viwango vyao kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara.