Yves Bissouma
KIUNGO mkabaji wa Brighton, Yves Bissouma ameibuka kama mlengwa mkubwa wa Liverpool.
Kulingana na Sunday World, vyanzo huko Brighton vimewaambia kuwa kijana huyo wa miaka 24 anafahamu maslahi kutoka Anfield.(Mail).

Robert Lewandowski
WAKALA wa Robert Lewandowski,anaangalia kufanya mazungumzo na Bayern Munich.
Kulingana na Sport 1, chaguzi zote ziko kwenye meza ikiwemo ya kuongeza mkataba au uwezekano wa kuondoka kwa nyota huyo wa Poland.(Goal).

Lionel Messi
DANI Alves amebainisha amemwambia, Lionel Messi, kubakia Barcelona.
Hatma ya Messi huko Barca iko mashakani, na mkataba wake unamalizika, lakini, Alves amesema nyota huyo wa Argentina anaweza kuachana na klabu hiyo.(Goal).

Markus Krosche
MARKUS Krosche amethibitishwa kama mkurugenzi mpya wa michezo wa Eintracht Frankfurt.
Krosche atachukua nafasi ya Fredi Bobic na klabu hiyo imefurahishwa na uteuzi wao mpya.(AP).

Victor Valdes
VICTOR Valdes anarejea Barcelona.
Rais mpya wa Barca, Joan Laporta ni shabiki mkubwa wa mkongwe huyo wa Camp Nou, na anawekwa kumsimamia kama kocha wa makipa wa vijana wa klabu.(Goal).

Joe Willock
MATUMAINI ya Newcastle ya kumsaini, Joe Willock, yameota mbawa na Mikel Arteta anaangalia kwa ajili yake kumpa nafasi Arsenal.
Willock amekuwa na kiwango cha kuvutia ‘Tyneside’ tangu ajiunge kwa mkopo mnamo Januari, na Magpies wanataka uhamisho wa kudumu. (Goal).

Jadon Sancho
MATUMAINI ya Liverpool kumsajili, Jadon Sancho, yanategemea klabu hiyo kupata nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bosi wa wekundu hao, Jurgen Klopp ni shabiki mkubwa wa winga huyo wa Borussia Dortmund, ambaye analengwa na Liverpool kama chaguo la kwanza.(Bild).

Ralf Rangnick
KLABU ya Tottenham wamemgeukia, Ralf Rangnick kama mrithi wa Jose Mourinho.
Bosi huyo wa Ajax, Eric ten Hag aliaminika kuwa chaguo la kwanza la Spurs, lakini, akaongeza mkaba wake huko Amsterdam.

Neymar
LENGO la Neymar ni kurudi Barcelona, kulingana na RAC1.
Rais mpya wa Barcelona, Joan Laporta anataka kumrudisha Mbrazil huyo Camp Nou, na mshambuliaji huyo ana hamu ya kuungana tena.

Edinson Cavani
MSHAMBULIAJI, Edinson Cavani atafanya uamuzi juu ya hatma yake katika siku zijazo.
Nyota huyo ana chaguo la kuongeza kandarasi yake ya Manchester United kwa msimu mmoja zaidi, au anaweza kuondoka msimu wa joto.(Goal).