ZASPOTI

Kamaldeen Sulemana
KLABU ya Ajax imejiunga na Manchester United katika kinyang’anyiro cha nyota wa Ghana, Kamaldeen Sulemana.
Sulemana (19), kwa sasa anaichezea Nordsjaelland ya Denmark ambaye alikataa ofa ya pauni milioni 10 ya huduma yake kutoka Ajax mnamo Januari. (Goal).

Konstantinos Mavropanos
KLABU ya Stuttgart ina azma ya kushikilia beki wa Arsenal, Konstantinos Mavropanos.
Klabu hiyo ya Ujerumani tayari iko kwenye mazungumzo na maofisa wa washika bunduki juu ya kuongeza mkataba wa mkopo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa mwaka mmoja zaidi.(Kicker).

Bruno Fernandes
NYOTA wa Manchester United, Bruno Fernandes, atashuhudia mfuko wake wa mshahara ukijaa mara mbili kwa ukubwa wakati wa kiangazi.
Fernandes amethibitisha kiwango bora kwa mashetani wekundu tangu ajiunge nao akitokea Sporting, na klabu hiyo sasa itasukuma mshahara wake hadi pauni 200,000 kwa wiki ili kumfunga Old Trafford. (Sun).

Edinson Cavani
KLABU ya Manchester United inafikiria makubaliano mapya yenye faida kubwa ya kumshawishi, Edinson Cavani, abakie.
Raia huyo wa Uruguay, ambaye analengwa na wababe wa Argentina wa Boca Juniors, anaweza kushuhudia mshahara wake ukiongezeka hadi pauni 250 kwa wiki ili kucheza kwa mwaka mwengine kwenye Ligi Kuu ya England. (Sun).

Gabby Agbonlahor
BEKI, Gabby Agbonlahor, anatumai kuwa mkopo wa nyota wa zamani wa Aston Villa, Axel Tuanzebe, unaweza kumshawishiwa kurudi Birmingham katika dirisha lijalo la uhamisho.
“Yeye ndiye aina ya mchezaji ambaye anaweza kushinikiza beki ya kati ya Villa kwa sasa,” Agbonlahor.(Soccer Insider).

Eric Dier
KOCHA mpya wa Roma, Jose Mourinho, ameambiwa anaweza kusahau juu ya kuimarisha kikosi chake kwa uvamizi dhidi ya Tottenham.
Bosi huyo wa zamani wa Spurs ana nia ya kumleta, Eric Dier na Pierre-Emile Hojbjerg katika mji mkuu wa Italia, lakini, miamba hiyo ya London wanasisitiza kwamba wawili hao hawauzwi. (Sun).

Jadon Sancho
MANCHESTER United itamfanya Jadon Sancho kuwa kipaumbele cha juu cha uhamisho wakati wa msimu wa joto.
Wekundu hao wanapanga dau la pauni milioni 80 kwa Sancho, huku wakipunguza azma yao kwa mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund, Erling Haaland ambaye amepewa thamani ya hadi pauni milioni 150 na yuko nje ya bei ya klabu hiyo. (Daily Star).

Odsonne Edouard
KLABU ya Leicester City imeongeza harakati zao za kumtafuta nyota wa Celtic, Odsonne Edouard.
Hatma ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa huko Parkhead haijulikani, na Bhoys bado hawajataja mbadala wa meneja wa zamani, Neil Lennon. (Daily Record).

Harry Kane
NYOTA wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane, ataitaka klabu yake kufikiria kusikiliza ofa za huduma zake msimu huu wa joto.
Moja ya klabu inayomuwania mshambuliaji huyo wa England ni Manchester United, ambayo wanapanga ofa kubwa ya kumuongeza kwenye safu yao ya mbele. (Sun).