MBAPE
KLABU ya PSG inajipanga kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 28, endapo mshambuliaji wao tegemezi Kylian Mbappe ataamua kutokuongeza mkataba wake. (Mirror)
JULIAN DRAXLER
KIUNGO wa PSG na Ujerumani Julian Draxler, 27, amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo kabla ya mkataba wake wa sasa kufikia tamati mwishoni mwa msimu. (Le Parisien)
RAFAEL BORRE
KLABU ya Watford ambayo ipo mbioni kupanda katika ligi ya England ipo katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Colombia Rafael Borre, 25, ambaye mkataba wake na miamba ya Argentina klabu ya River Plate unafikia tamati mwishoni mwa msimu. (Sun)
BRUNO FERNANDES
KIUNGO wa Ureno Bruno Fernandes anatarajiwa kupatiwa mkataba mpya ambao mshahara wake utapandishwa mara mbili kufikia pauni 200,000 kwa wiki na klabu yake ya Manchester United baada ya fainali ya Kombe la Europa. (Sun)
ROY HODGSON
KOCHA wa Crystal Palace Roy Hodgson anaamini kuwa klabu hyo itambakiza kiungo raia wa England Eberechi Eze, 22, kwa msimu wa 021-22 licha ya mchezaji huyo kuvivutia vilabu mbalimbali. (Goal)
JOSE MOURINHO
TOTTENHAM wamemuonya kocha wao wa zamani Jose Mourinho asijaribu beki wa England Eric Dier, 27, na kiungo wa Denmark, 25, Pierre-Emile Hojbjerg mara atakapoanza kuinoa klabu ya Roma mwishoni mwa msimu.
RENAN LODI
KLABU ya Lyon could inaweza kutuma ofa ya usajili kwa klabu ya Atletico Madrid ili kumnasa beki wake Mbrazili Renan Lodi, 23. (L’Equipe)
ARTURO VIDAL
KLABU ya Inter Milan itapokea ofa za usajili kwa kiungo Arturo Vidal, 33, kama sehemu ya mpango wa klabu hiyo kupunguza mlima wa mishahara, na japo klabu Marseille imehusishwa na kutaka kumsajli raia huyo wa Chile, hakuna maombi rasmi yaliyotumwa. (Calcio Mercato – in Italian)