WILLIAN
WINGA wa Brazil Willian anatarajiwa kuondoka Arsenal mwisho wa msimu huu , lakini The Gunners haijapokea maombi yoyote ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Fabrizio Romano, via Mail)
YOURI TIELEMANS
KIUNGO wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans atafanya mazungumzo ya mkataba mpya na Leicester mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alifunga bao la ushindi katika fainali ya FA dhidi ya Chelsea , ana miaka miwili iliosalia katika mkataba wake. (Mail)
MASSIMILIANO ALLEGRI
ALIYEKUWA kocha wa Juventus Massimiliano Allegri anaonekana kuwa kipaumbele katika kuchukua nafasi ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane badala ya aliyekuwa mshambulia hatari wa timu hiyo Raul kuwa kocha mpya wa klabu hiyo. (Marca)
XAVI
BARCELONA imeanza mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Al Saad ya Qatari Xavi kuchukua kuchukua nafasi ya Ronald Koeman kama kocha mpya wa klabu hiyo ya NouCamp. (ARA Esports, via Football Transfers)
SVEN BOTMAN
BEKI wa Netherlands Sven Botman, ambaye alihusishwa na uhamisho wa kuelekea Liverpool mwezi Januari , anasema kwamba ligi kuu ina kitu maalum , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliongezea kwamba anafurahia kwa sasa katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Athletic – subscription required)
TOBY ALDERWEIRELD
BEKI wa Tottenham Toby Alderweireld analengwa na klabu ya Ubelgiji Club Bruges lakini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji hatafanya uamuzi kuhusu hatma yake hadi atakapojua ni nani atakayechukua nafasi ya ukocha wa klabu hiyo kutoka kwa kaimu meneja wa Spurs Ryan Mason. (Voetbal 24, via Express)
JACOB MURPHY
LEEDS UNITED na Burnley wamejiunga na klabu ya Southampton, Watford na Rangers katika kutaka kumsaini winga wa Newcastle Jacob Murphy, 26. (Football Insider)
RADU DRAGUSIN
CRYSTAL PALACE inatumai kumsaini beki wa Romania mwenye umri wa miaka 19 Radu Dragusin kwa mkopo kutoka kwa klabu ya Juventus nchini Itali. (Sun)
HAKAN CALHANOGLU
KIUNGO wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu ambaye mkataba wake unakamilika tarehe 30 mwezi Juni katika klabu ya AC Milan, anasema kwamba hatma yake haitegemei timu hiyo kutinga ligi ya mabingwa Ulaya na kwamba atajadili hali yake nao mwisho wa msimu huu. (Sky Sport Italia, via Football Italia)
GIOVANNI CARNEVALI
MKURUGENZI wa klabu ya Sasuolo Giovanni Carnevali anasema kwamba haiwezekani kabisa kwamba kiungo wa kati wa Itali, Manuel Locateli atasalia katika klabu hiyo ya Serie A msimu ujao, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuhusishwa na baadhi ya klabu. (Sky Sport Italia, via Football Italia)