HARRY KANE

MSHAMBULIAJI wa England Harry Kane kwa mara nyengine ameambia Tottenham anataka kuondoka katika klabu hiyo ya ligi kuu mwisho wa msimu huu. Manchester City, Chelsea na Man United zimeonesha hamu ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Sky Sports)

NUNO MENDES

MANCHESTER UNITED itashindana na Manchester City katika ununuzi wa beki kinda wa Sporting Lizborn Nuno Mendes kwa dau la £52m. (Mail)

SANTIAGO MORENO

LEEDS UNITED na mabingwa wa Uskochi Rangers wanamchunguza mchezaji wa klabu ya America de Cali mwenye umri wa miaka 21 raia wa Colombia Santiago Moreno. (Football Insider)

KIERAN TRIPPIER

MCHEZAJI wa England Kieran Trippier amehusishwa na hatua ya kurudi katika ligi kuu  , huku Manchester United na Everton zote zikishindana kupata saini ya beki huyo wa kulia kutoka Atletico Madrid. (Athletic, subscription required)

YVES BISSOUMA

KLABU ya Brighton & Hove Albion imeambia Liverpool na Arsenal itachukua dau la pauni milioni 40 kumsaini kiungo wa kati wa Mali mwenye umri wa miaka 24 Yves Bissouma. (Sun)

KAMALDEEN SULEMANA

MANCHESTER UNITED inaiongoza Ajax katika mbio za kumsaini mshambuliaji wa Ghana Kamaldeen Sulemana kutoka FC Nordsjaelland baada ya mazungumzo ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 siku ya Jumatatu.. (Football Insider)

MARCOS ALONSO

BEKI wa Uhispania Marcos Alonso, 30, na beki wa kushoto wa Itali mwenye umri wa miaka 26 Emerson Palmieri wanapigania kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu ili kujaribu kutafuta fursa katika ligi ya Serie A , kwa kuwa wote wanataka kuhisi kwamba wao ni muhimu kwa mara nyengine.

PATRICK VAN AANHOLT

BEKI wa Uholanzi Patrick van Aanholt, 30, anatarajiwa kuondoka Crystal Palace wakati mkataba wake utakapokamilika (Athletic, subscription required)

MEMPHIS DEPAY

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 27, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Barcelona kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu. (L’Equipe – in French)

GERVINHO

MCHEZAJI wa Ivory Coast na aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Gervinho, 33, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Itali ya Serie A Parma mwisho wa mkataba wake ili kujiunga na klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Goal – in Turkish)