Emiliano Buendia
ARSENAL wameongeza juhudi za kumsajili kiungo wa Argentina, Emiliano Buendia (24), kutoka Norwich City huku miamba hiyo ikitaka kuziba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Norway, Martin Odegaard (22), ambaye yuko tayari kurudi Real Madrid mwishoni mwa kipindi chake cha mkopo.(Mail).

Harry Kane
MANCHESTER City wapo tayari kuwashinda Manchester United na Chelsea kuipata sahihi ya mshambuliaji wa Uingereza, Harry Kane (27) ambaye anasisitiza Tottenham haiwezi kumzuia kuondoka.(Star).

Raheem Sterling
MABINGWA wa England, Manchester City wamepania kumpa mshambuliaji wa England Raheem Sterling (26), mkataba mpya wa kudumu.(Telegraph).

Gareth Bale
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid wa Wales, Gareth Bale (31), anaweza kuongeza muda wake wa mkopo na Tottenham kwa mwaka mwengine ikiwa Kane atapewa ruhusa ya kuondoka klabuni humo.(AS).

Adam Armstrong
WEST Ham na Fulham zinaongoza harakati za kumsajili mshambuliaji wa England anayekipiga Blackburn Rovers, Adam Armstrong ambaye thamani yake ni pauni milioni 25, lakini, klabu hizo za London zinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Brighton na Everton.(Sun).

Chris Wilder
KLABU ya West Bromwich Albion ipo tayari kuanza mazungumzo na bosi wa zamani wa Sheffield United, Chris Wilder (53), juu ya kuchukua nafasi ya meneja anayemaliza muda wake Sam Allardyce. (Telegraph).

Niklas Sule
KOCHA wa Chelsea, Thomas Tuchel, bado ana azma ya kumsajili beki wa Bayern Munich na Ujerumani, Niklas Sule (25). (Abendzeitung).

Kamaldeen Sulemana
MANCHESTER United imeweka wazi kwa FC Nordsjaelland kwamba wako tayari kuizuia Ajax kumsajili mshambuliaji wa Ghana mwenye umri wa miaka 19, Kamaldeen Sulemana.(Football Insider).

Adama Traore
WINGA wa Wolves, Adama Traore (25), yuko kwenye mazungumzo juu ya kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England na kukomesha uvumi unaomhusisha mchezaji huyo wa Hispania na Liverpool na Barcelona.(Goal).

Gianluigi Buffon
KIPA wa Italia mwenye umri wa miaka 43, Gianluigi Buffon, amesema, kustaafu ni chaguo kwake wakati mkataba wake huko Turin utamalizika katika msimu wa joto, lakini, amesisitiza atasaka changamoto nyengine ya wazimu. (Rai Sport).

Boubakary Soumare
KLABU ya Leicester City wanakaribia kumaliza mkataba wa miaka minne wenye thamani ya jumla ya euro 25 kwa kiungo wa Ufaransa wa Lille, Boubakary Soumare (22). (Julien Laurens on Twitter).

Joe Willock
KLABU ya Newcastle United wanajiandaa kumsajili kiungo wa England chini ya miaka 21, Joe Willock kwa mkataba wa kudumu kutoka Arsenal, makubaliano ambayo pia yanaweza kusaidia kumshawishi winga wa Ufaransa, Allan Saint-Maximin abakie St. James Park. (Telegraph).

Ebrima Darboe
KLABU za Arsenal na Tottenham zinavutiwa na kiungo wa Roma raia wa Gambia mwenye umri wa miaka 19, Ebrima Darboe, ambaye amecheza mara tano na klabu hiyo ya Italia (Corriere dello Sport).

Charlie Austin
KLABU ya Queens Park Rangers wanatarajia kumaliza makubaliano ya kumbakisha mshambuliaji wa England, Charlie Austin (31), baada ya kiungo, Sam Field (23), ambaye pia alikuwa kwa mkopo kutoka klabu hiyo kukamilisha uhamisho wake wa kudumu kwenda Loftus Road. (West London Sport).

Jack Harrison
KLABU ya Leeds United wamepanga kutumia kifungu cha kugeuza uhamisho wa mkopo wa winga wa England, Jack Harrison kutoka Manchester City kuwa mkataba wa kudumu.(Football Insider).

Tom Heaton
MANCHESTER United wapo tayari kumsajili tena mlinda mlango wa England, Tom Heaton (35) kwa uhamisho wa bure kutoka Aston Villa. Muingereza, Sam Johnstone (28), ambaye alikuwa mlengwa mwengine atahamia West Ham kutoka West Bromwich Albion.(Talksport).

Miralem Pjanic
KLABU ya Chelsea na Paris St-Germain wanafikiria kumchukua kiungo wa kati wa Bosnia mwenye umri wa miaka 31, Miralem Pjanic. (Le10Sport).