THOMAS TUCHEL
KOCHA wa Chelsea Thomas Tuchel anamtaka mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, lakini the Blues wanahofu kuwa mahasimu wao wa magharibi mwa London watakataa kumtoa. (Telegraph, subscription required)
TONY CASCARINO
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Tony Cascarino ameidokezea Tottenham kumfukuzia mshambuliaji wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 25 Ollie Watkins ili awe pacha wake endapo Kane ataondoka Spurs. (Talksport)
MARCELO BIELSA
LEEDS UNITED wamekubali kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja na kocha wao raia wa Argentina Marcelo Bielsa mwenye umri wa miaka 65, huku tangazo rasmi likitarajiwa kutolewa wiki hii. (Mirror)
CRISTIANO RONALDO
KLABU ya Manchester United inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji mshambuliaji wake wa zamani Cristiano Ronaldo wa Juventus, huku “mawakala wanaofahamiana” na mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka, 36, wakiesema “anaweza kutaka kuondoka ” katika klabu hiyo ya Turin. (Athletic, subscription required)
YVES BISSOUMA
MATUMAINI ya Liverpool ya kusaini mataba na kiungo wa Mali Yves Bissouma mwenye umri wa miaka 24 kutoka Brighton, yamepigwa jeki na uamuazi wa Arsenal wa kuendelea kutafuta atakayemrithi. (Mail)
IBRAHIMA KONATE
WAKATI huo huo, nia ya Liverpool ya kumtaka mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate, 21, imekuwa ngumu kutokana na utashi wa klabu hiyo ya Bungasliga wa kuwa na kipengele za kumuachilia cha thamaini ya pauni milioni 34 ambacho wanataka kilipwe chote- kwa hiyo Reds wanaweza kumuendea beki wa Uturuki Ozan Kabak, 21. (Times, subscription required)
GEORGE WIJNALDAM
PARIS ST-GERMAIN ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, ambaye anaondoka Liverpool kama mchezaji huru. Barcelona bado hawajaweka dau kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Le10Sport – in French)
MIKEL ARTETA
MENEJA wa Arsenal Mikel Arteta anasema Arsenal itaanza mazungumzo na Real Madrid kuhusu mkataba mpya kwa ajili ya kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo Martin Odegaard, 22, “katika wiki chache zijazo “. (Sun)
JUAN MATA
KIUNGO mchezeshaji wa Manchester United, Juan Mata hana hakika kama ataendelea kusalia katika klabu hiyo baada ya kuisha kwa mkataba wake katika majira ya joto ya mwaka huu.
DANIEL FARKE
MENEJA wa Norwich City Daniel Farke anasema atahitaji “kuchukua mwelekeo wa hatari zaidi kuliko klabu nyingine” katika soko la uhamisho iwapo wanataka kusalia katika Ligi ya Primia msimu ujao.(Eastern Daily Press)
ROBIN GOSENS
BARCELONA wamekuwa na nia ya kumchukua kiungo wa nyuma-kushoto wa Atalanta na Ujerumani Robin Gosens, 26, ambaye amekuwa akihusishwa pia na Manchester City, Inter Milan, Juventus na AC Milan. (Sport – in Spanish)
ZINEDINE ZIDANE
ZINEDINE Zidane atafanya maziungumzao na Real Madrid katika siku zijazo kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo. (ESPN)
DANI CEBALLOS
REAL MADRID wataangalia jinsi ya kumuuza kiungo wa safu ya kati Muhispania Dani Ceballos msimu huu, lakini Arsenal hawatataka mkataba wa kudumu kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 24. (90min)