Antonio Conte
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte ambaye ameachana na Inter Milan, anataka kujiunga na Tottenham Hotspurs. (Guardian).

Ole Gunnar Solskjaer
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu, licha ya United kupoteza mechi ya fainali ya Kombe la Europa dhidi ya Villarreal. (Telegraph).

Andrea Pirlo
KLABU ya Juventus inatarajiwa kumrejesha kocha wao wa zamani, Massimiliano Allegri baada ya kumfuta kazi, Andrea Pirlo. (Guardian).

Simone Inzaghi
KOCHA, Simone Inzaghi anatarajiwa kutangazwa kuinoa Inter Milan baada ya kuachana na Lazio. (Athletic).

Granit Xhaka
KOCHA wa zamani wa Tottenham Hotspurs, Jose Mourinho anataka kiungo wa Uswizi na Arsenal, Granit Xhaka (28), kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili akiwa Roma. (Sky Italy).

Nikola Milenkovic
BEKI wa kati wa Fiorentina, Mserbia Nikola Milenkovic (23), ni pendekezo namba moja anayelengwa na Borussia Dortmund. (Sky Sports German).

Paulo Dybala
MUSTAKABALI wa mshambuliaji wa Argentina, Paulo Dybala kuendelea kuwachezea mabingwa wa Ligi ya Serie A, Juventus haujulikani na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuuzwa msimu huu. (Mirror).

Dean Henderson
TOTTENHAM na Borussia Dortmund wanaongoza katika mbio za kumsajili mlinda mlango wa Manchester United, Dean Henderson (23). (Sky Sports).

Erling Braut Haaland,
CHELSEA inaamini kwamba itamsajili mshambuliaji wa Norway, Erling Braut Haaland (20) kutoka Borussia Dortmund majira ya joto. (Eurosport).

Thomas Tuchel
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich atampa kocha, Thomas Tuchel, kiasi cha pauni milioni 260 kutumia wakati wa dirisha lijalo la usajili, bila ya kujalli kama klabu itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Tutto Mercato).

Declan Rice
KLABU ya West Ham itasikiliza ofa iliozidi pauni milioni 100 ili kumuachia kiungo wa kati wa England, Declan Rice (22). (Talksport).

Andre Silva
MANCHESTER United inaweza kupatiwa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Mreno Andre Silva (25), wakati wa dirisha la usajili msimu wa joto. (Sun).

Reiss Nelson
KLABU ya Arsenal itasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo, Reiss Nelson (21), mwishoni mwa msimu. (CBS).

Miguel Azeez
ARSENAL pia wako kwenye mazungumzo na mchezaji wao kinda, Miguel Azeez (18), kuhusu mkataba wa muda mrefu (Sun).