CRISTIANO RONALDO

MANCHESTER UNITED wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo huku klabu hiyo ya Italia ikiwa iko tayari kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 36 kwa kubadilishana na kiungo wa kati Paul Pogba , 28. (Gazzetta dello Sport via Express)

GABRIEL JESUS

TOTTENHAM wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus,24, ambapo itashuhudia kubadilishana na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane,27, pamoja na nyongeza ya fedha.(Star)

DANI CEBALLOS

KIUNGO wa kati Dani Ceballos, 24, amesema anataka kusalia Real Madrid msimu ujao au kuondoka kabisa kwenye klabu baada ya kutumia misimu miwili akichezea klabu ya Arsenal (Mail)

JOE WORRALL

BURNLEY wamepanga kutoa zabuni ya pauni milioni 10 kwa ajili ya mlinzi wa kati Joe Worrall,24. (Sun)

SAM ALLARDYCE

KOCHA wa zamani wa England ma Crystal Palace yuko kwenye orodha ya kuchukua nafasi ya ukufunzi kwenye klabu ya West Brom baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce. (Mirror)

MAURICIO POCHETTINO

TOTTEHNAM wana mpango wa kuanza mazungumzo rasmi na Paris St-Germain siku ya Jumatatu ukiwa mpango wa kumrejesha Mauricio Pochettino kwenye klabu. (Sun)

STEVEN BERGWIJN

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Steven Bergwijn anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa joto huku Ajax ikiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo, 23.(De Telegraaf)

DOUGLAS LUIZ

ASTON VILLA wana hofu ya kumpoteza kiungo wao nyota Douglas Luiz ,23, huku timu yake ya zamani ya Manchester City ikihitaji kumsajili tena Mbrazili huyo.(90 Min)

FIKAYO TOMORI

AC MILAN wataanza mazungumzo na Chelsea Jumatatu kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa England Fikayo Tomori,23 kwa mkataba wa kudumu. (Sport Witness)

JOSE MOURINHO

ARSENAL imemwambia kocha wa Roma Jose Mourinho kuwa wanahitaji pauni milioni 17 kwa ajili ya kiungo wa kati Granit Xhaka, 28. (Gazzetta dello Sport)

HARRY WILSON

LEEDS hawana mpango tena wa kumnyakua kiungo wa kati wa Liverpool Harry Wilson msimu huu wa joto. (Football Insider)

JOSE MOURINHO

ARSENAL imemwambia kocha wa Roma Jose Mourinho kuwa wanahitaji pauni milioni 17 kwa ajili ya kiungo wa kati Granit Xhaka

TONY BLOOM

MWENYEKITI wa Brighton Tony Bloom yuko tayari kusikiliza ofa za wachezaji kama kiungo wa Mali Yves Bissouma, 24, na mlinzi wa Kiingereza Ben White, 23, huku wakizivutia Arsenal, Liverpool na Manchester United. (The Athletic)

TOM DAVIES

SOUTHAMPTON wana mpango kumsajili kiungo wa Everton Tom Davies baada ya mwaka jana kushindwa kumsajili Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22.(Football Insider)

DIOGO DALOT

MCHEZAJI wa Manchester United Diogo Dalot amekiri kuwa hajui mustakabali wake baada ya kiungo huyo wa kati,22, kucheza kwa mkopo AC Milan msimu uliopita. (Manchester Evening News)