NA HAJI NASSOR, PEMBA
HISTORIA inatuonesha kuwa, baada ya vita vikuu vya dunia mwaka 1945, mataifa makubwa duniani yalikutana kwa lengo la kuumizwa vichwa, kutokana na uvunjaji wa haki binaadamu.
Katika vita hivyo, wanawake na watoto walikuwa ni waathirika wakubwa kwa kufanyiwa ukatili wa kutisha na hivyo kutokana na hali hiyo, mataifa kadhaa yaiungana kwa lengo la kupiga vita udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.
Sambamba na hilo, lakini nchi hizo kwa umoja wao walitoa tamko hilo kwa ulimwengu la haki za binaadamu la mwaka 1948.
“Binadamu wote huzaliwa wakiwa huru na sawa katika utu na haki zao’’ ambapo Ibara hii ndio msingi wa harakati za ukombozi wa haki za binadamu.
Na ndio maana, historia zinatueleza mwaka 1979 baraza kuu la umoja wa mataifa ililipitisha mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi, dhidi ya mwanamke (CEDAW) na mkataba kuanza kutumika mwaka 1981.
Kufuatia hali hiyo nchi wanachama ikiwemo Tanzania uliuridhia na kufanya marekebisho katika katiba yake.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, imeelezea haki na usawa katika kifungu cha 11 (1), ambacho kinaeleza kuwa, ‘binadamu wote huzaliwa wakiwa huru na ndioa maana kila mtu anastahiki heshima ya kutambuliwa utu wake’.
Hata hivyo, Sheria ya mtoto namba 6 ya mwaka 2011 ya Zanzibar, imetamka bayana kuwa ‘mtoto ni mtu aliechini ya miaka 18’ kama hivyo ndivyo basi wapo waliochini ya miaka hiyo, hutelekezwa na familia zao.
Mama mmoja 40 mkaazi wa Tibirinzi wilaya ya Chakechake Pemba, alieachwa na watoto sita, watano wakiwa wa kike na watatu kupewa ujauzito na kisha kuolewa hata kabla ya kumaliza masomo.