MADRID, Hispania

KOCHA wa timu ya Taifa ya soka ya Hispania Luis Enrique ametangaza kikosi chake kuelekea michuano ya Euro 2020 inayotarajiwa kuanza Juni 11, 2021 huku akimtema nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos.

Pia kwenye orodha ya wachezaji hao 24 hakuna jina la mchezaji hata mmoja anayecheza ndani ya Real Madrid.

Enrique amesema  hana tatizo na kocha mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane ila amechagua wachezaji kwa namna alivyoona inafaa.

“Kama Dani Carvajal na Ramos wangekuwa fiti nina amini kwamba wangekuja. Siwezi kuweka orodha yangu kama hivyo,” .

Orodha kamili ya wachezaji ambao wameitwa.

Makipa: Unai Simon (Athletic Bilbao), David de Gea (Manchester United), Robert Sanchez (Brighton)

Mabeki: Pau Torres (Villarreal), Aymeric Laporte (Manchester City), Diego Llorente (Leeds United), Eric Garcia (Manchester City), Jordi Alba (Barcelona), Jose Gaya (Valencia) Cesar Azpilicueta (Chelsea)

Viungo: Sergio Busquets (Barcelona) Rodri (Manchester City), Thiago Alcantara (Liverpool), Pedri (Barcelona), Marcos Llorente (Atletico Madrid), Koke (Atletico Madrid), Fabian Ruiz (Napoli)

Washambuliaji: Gerard Moreno (Villarreal), Ferran Torres (Manchester City), Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Alvaro Morata (Juventus), Dani Olmo (RB Leipzig), Pablo Sarabia (Paris Saint-Germain), Adama Traore (Wolves) .