ZASPOTI
WAKALA, Jorge Mendes, amesema, Cristiano Ronaldo, hana mpango wa kurudi Sporting CP msimu huu wa joto.

Hatma ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 huko Juventus inazidi kutokuwa na uhakika na uvumi ukiendelea huku anajiandaa kuingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake huko Turin.

Baadhi ya uvumi huo ulidokeza kwamba mshambuliaji huyo anaweza kurudi kwenye klabu yake ya ujana ya Sporting, ingawa Mendes amehamia haraka kukana madai hayo.
Alikuwa mama wa Ronaldo, Dolores Aveiro ambaye alisaidia kukuza uvumi juu ya kurejea Sporting mapema wiki hii.

Akizungumza na mashabiki juu ya hatma ya mtoto wake kutoka makaazi yake wakati wakisherehekea mafanikio ya kwanza ya Sporting Liga tangu 2002, alisema: “Nitazungumza naye kumrudisha. Mwaka ujao atacheza Alvalade [uwanja wa Sporting]”.(Goal).