NA VICTORIA GODFREY

WANARIADHA saba Zanzibar wanatarajia kushiriki  Mashindano ya majaribio ya kufuzu kushiriki Olimpiki  itakayofanyika mwaka huu Tokyo,Japani.

Mashindano ya majaribio yanatarajia kuanza kutimua vumbi June 17 na 18 mwaka huu nchini Kenya.

Akizungumza na gazeti hili Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha Zanzibar Yasin Muhidi,alisema kati ya hao wanawake wanne na wanaume watatu.

Alisema wanaendelea   mazoezi ya nguvu ya kuhakikisha wanakwenda kufanya vizuri waweze kupata matokeo mazuri katika majaribio hayo.

” Kwa sasa tunaendelea na maandalizi na mwanzo tulikuwa na wanariadha wa nne ,lakini tumeongeza nguvu ya wengine mmoja kwa wanaume na wawili kwa upande wa wanawake,tunaimani watajipanga na kwenda kufanya vizuri,” alisema Muhidini.

Aliwataja wanariadha hao wanaume ni Ali Hamis Gulam( mita 100,200)Sinai Kombo na Twahir Twahir watakimbia mita 400,wakati wanawake Jane Maige, Emmy Hosea Andi,Winfrida Machengi  na Aines John wakiwa chini ya kocha Mkuu Nyange Kombo Haji  na Msaidizi Mohamed Abdi  Shoka