Vifaa tiba, kinga, dawa bado vyahitajika zaidi

NA MOHAMMED SHARKSR (SUZA)

LEO dunia inaadhimisha siku ya Wauguzi ambapo kila ifikapo Mei 12 ya kila mwaka wauguzi wa Zanzibar wanaungana na wauguzi wenzao duniani kuadhmisha siku hiyo.

Kwa Zanzibar Baraza la Wauguzi na Wakunga likishirikiana na Jumuiya ya Wakunga Zanzibar (ZANA) wameungana na wauguzi na wakunga wenzao katika siku ya maadhimisho hayo.

Lengo kubwa la siku ya wauguzi duniani ni kutoa mwamko kwa wananchi juu ya mchango wa wauguzi na wakunga katika jamii na kuwa pamoja nao.

Sambamba na hilo, lakini kutoa huduma kwa wagonjwa, kushirikishwa katika ngazi mbalimbali za uongozi na ngazi za maamuzi kwa lengo la kuwaendeleza Wauguzi katika elimu sahihi.

Kimataifa bado kuna dhana potofu zilizopo katika jamii kwamba wauguzi na wakunga wanatabia ya kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wagonjwa au wateja wao.

Ni wazi kuwa bado waguzi na wakunga wana changamoto nyingi wanazozipata pindi wanapokuwa katika sehemu zao za kazi kama vile uhaba wao, manyanyaso  kutoka kwa wagonjwa na wanajamii.

Hakuna asiejua kuwa mchango wa kada za uuguzi hapa Zanzibar na dumiani kwa ujumla ni mkubwa kiasi ambacho watumishi wa kada hizi hufanyakazi masaa 24 kila siku kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa zaidi ya asilimia mia 80 ya huduma zote za afya.

Makala haya ilizungumza na baadhi ya wauguzi na kueleza namna wanavyotekeleza majukumu yao.