KARACHI, PAKISTAN

WAZIRI Mkuu wa Pakistani, Imran Khan, leo yuko ziarani nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kujadili ushirikiano baina ya nchi mbili hizo.

Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya mambo ya nje ya Pakistan ilisema kuwa akiwa ziarani huko atakutana na mrithi wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman bin Abdulaziz Al Saud.

Sambamba na hilo lakini, Khan akiongozana na ujumbe wake akiwa ni pamoja na wizara ya mambo ya nje wa Pakistan Shah Mahmood Qureshi pamoja na mawaziri wengine watajadili masuala ya pamoja baina ya nchi mbili hizo.

Waziri mkuu akiwa Saudia watajadili masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika uchumi, biashara, uwekezaji, fursa za ajira, nishati sambamba na kuzzungumza na wanadiaspora wa Pakistan wanaoishi Saudia.

Ziara hiyo ya siku tatu pia itagusia masuala ya kikanda, kimataifa na masuala mengine yanayohusu maslahi ya nchi mbili hizo.