NA MWANDISHI WETU
KIKOSI cha Yanga jana Mei 18 kimewasili salama makao makuu ya Tanzania, Dodoma na kupata fursa ya kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna vikao vya Bunge ambavyo vinaendelea.
Yanga ilianza safari jana Mei 18 asubuhi kuibukia Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa ligi kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, leo Mei 19 majira ya saa 10:00 jioni.
Kupitia ukurasa wao rasmi wa Isntagram, Yanga waliandika namnai:”Timu ya mabingwa wa kihistoria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”.
Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga iliondoka na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.
Hivyo mchezo huo utakuwa na ushindani kwa timu zote mbili ambapo JKT Tanzania watahitaji kulipa kisasi na Yanga wao kulinda rekodi zao.
Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 58 inawafuata JKT Tanzania walio nafasi ya 13 na pointi 33.