NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefaya uteuzi wa viongozi wa wakurugenzi katika taasisi mbalimbali za serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, ilieleza kuwa Dk. Salha Mohammed Kassim ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Mwinyi amemteua Sheikha Ahmed Mohamed kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA).

Naye Makame Hasnu Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji Shirika la Meli na Uwakala (SHIPCO), ambapo Madina Haji Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe (STCDA).

Uteuzi wa viongozi hao umeanza rasmi Mei 10 mwaka huu.