NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika katika mbali mbali za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari na iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said, imeeleza kuwa viongozi walioteuliwa hapo jana ni pamoja na wakurugenzi na wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.

Katika uteuzi huo, Dk. Mwinyi amemteua Mshenga Mshenga Haidar kuwa meneja mkuu wa Shirkika la Umeme Zanzibar (ZECO).

Uteuzi mwengine ni Nassor Shaaban Ameir ameteuliwa kuwa Mkurugunzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Dk. Mwinyi amemteua Shariff Ali Shariff kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Dk. Huda Ahmed Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Suleiman Ame Khamis ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, ambapo Hartha Mohammed Ali ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.

Abdulla Mzee Abdulla ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, ambapo uteuzi wa viongozi hao wote umeanza jana.