BEIJING, CHINA

SHIRIKA la Afya duniani (WHO), limeitangaza China kuondokana na ugonjwa wa malaria, baada ya jitihada zilizodumu kwa takribani miaka 70 ya kuutokomeza ugonjwa huo unaosababishwa na mbu.

Taifa hilo ambalo liliwahi kuripoti zaidi ya visa milioni 30 vya maambukizi ya malaria katika miaka 1940, ambapo hivi sasa kwa zaidi ya miaka minne mfululizo hakuja ripotiwa mgonjwa yoyote wa malaria.

Tedros Adhanom Ghebreyesus

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa pongezi kwa China kwa hatua ya kuliondosha kabisa gonjwa hilo nchini mwao.

Katokana na hatua hiyo, China inaungana na mataifa mengine duniani ambayo yameonesha dunia bila malaria inawezekana.

China linakuwa taifa la 40 kutangazwa na WHO kuangamiza ugonjwa wa malaria, mataifa ya mwisho kupata hadhi hiyo ni El Salvador 2021, Algeria na Argentina 2019, Paraguay na Uzbekistan 2018.

Hivi sasa kuna orodha ya mataifa 61 ambayo malaria haipo kabisa au imetoweka bila ya kuwepo kwa mpango maalumu.