NA MWAJUMA JUMA

LIGI daraja la tatu wilaya ya Mjini juzi iliendelea katika viwanja vitatu tofauti na timu za Chemchem na Kiongochekundu wakishinda katika michezo yao.

Miamba hiyo yote ilishuka katika dimba la Mao Zedong A na B wakati wa  saa 7:30 za mchana, ambapo Kidongochekundu iliwafunga Rio Branco mabao 2-1 na Chemchem ikashinda kwa idadi kama hiyo ya mabao dhidi ya Azam Zanzibar.

Majira ya saa saa 10:00 uwanja wa Mao Zedong B Kwamtipura inayoongoza kundi A ,ilipunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Mpendae.

Kidongo chekundu katika mchezo wake huo mabao yake yalifungwa na Hija Ramadhan Iddi  dakika ya 19 na 82 na  Rio branco likafungwa na  Adul Juma Ali dakika ya  89, wakati  Mpendae ilicheza na Kwamtipura lilifungwa na  Juma Othman Haji  dakika ya 44.

Leo ligi hiyo itaendelea tena kwa kuchezwa mechi mbili ambapo katika uwanja wa Amaan kutakuwa na michezo miwili saa 8:00 na saa 10:00 na katika uwanja wa Mao Zedong itakuwepo miwili yote itachezwa saa 7:30 mchana katika uwanja wa Mao Zedong A na B.