NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika taasisi za serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said ilielezea kuwa Dk. Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya.

Aidha taarifa hiyo ya Mhandisi Zena ilifafanua kuwa Dk. Mwinyi amemteua Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Naye Arafat Ally Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC), ambapo uteuzi wa viongozi hao umeanza rasmi Juni 24 mwaka huu.