NA MWAJUMA JUMA

TIMU za soka za Greenada  na Kwamtipura zimetoa vichapo katika michezo yao ya ligi daraja la tatu iliyochezwa juzi kwenye viwanja tofauti.

Greenada ilishuka katika dimba la Amaan saa 10:00 za jioni kucheza na FC Rome na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, wakati Kwamtipura ilicheza katika uwanja wa Mao Zedong ilishinda mabao 4-2 dhidi ya Sicco.

Aidha katika uwanja wa Amaan saa 8:00 mchana Sapsoap na Chemchem zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.

Leo ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kwa kuchezwa mechi nne,uwanja wa Amaan nje Mwembenjugu itacheza na Enugu saa 7:30, saa 10:00 African Boys  itacheza na  Wondrous, Ziwatuwe na Sicco watacheza Mao Zedong B saa 7:30 na saa 10:00 Kwamtipura itapambana na Sebleni City.