NA JOSEPH DAVID

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa habari za mchezo Ali Mayay amempongeza kocha mkuu wa timu ya Yanga Mohamed Nasreddine Nabi kwa kusimamia nidhamu ya wachezaji katika kikosi hicho.

Mayay ametoa pongezi hizo baada ya klabu hiyo kuwasimamisha wachezaji wake akiwemo mlinda mlango Metacha Mnata, mlinzi wa kati na nahodha wa timu himu hiyo Lamine Moro pamoja na mshambuliaji Michael Sarpong.

Akionea kupitia redio ya Wasafi fm kwenye kipindi cha Mahakama ya michezo,  Mayay alisema kuwa inavyoonekana mambo ya utovu wa nidhamu kwenye kikosi hicho yalianza tangu mwanzo wa msimu kabla kocha huyu hajaja.

Aidha Mayay alisema suala la nidhamu halitakiwi kuwa na utashi wa mtu kwani ukiruhusu hali hiyo basi utovu wa nidhamu huibuka, hivyo uongozi wa klabu ndio unatakiwa kutoa muongozo kwa benchi la ufundi ili utekelezaji ufanyike.

Banchi la ufundi la Yanga lilitangaza kuwasimamisha nyota wake hao kutokana na sababu za utovu wa nidhamu kuelekea mechi yake dhidi ya Mwadui katika michuano na Azam Sports Federation (ASF) hatua ya robo fainali ambapo ilifanikiwa kusonga mbele kwa kuibuka na ushindi wa mabali 2-0, huku mfungaji wa mabao yote akiwa Deus Kaseke.