ZASPOTI. 
PAMOJA na Liverpool kuaminiwa kumsajili mshambuliaji wa Ghana mwenye umri wa miaka 17, Abdul Fatawu Issahaku kutoka Steadfast FC, rais wa klabu hiyo sasa amethibitisha kuuzwa kwake.
Wekundu hao walikuwa wakihusishwa na Fatawu Issahaku tangu mwisho wa Mei, wakati ilidaiwa walikuwa wakitafuta kuuteka nyara mpango wa Bayer Leverkusen kwa ajili ya Mghana huyo.

Ilielezwa baadaye kuwa Leverkusen ilikuwa imejitoa na Liverpool ilikuwa imehamia kwenye rada, kabla ya madai kwamba makubaliano yalifikiwa ya kumtoa mkopo Sporting CP hadi atakapopata kibali cha kufanya kazi nchini England.
Sasa, kulingana na taarifa za soka nchini Ghana, mmiliki na rais wa Steadfast FC, Haruna Iddrisu, amethibitisha uhamisho wa Fatawu Issahaku.
Iddrisu alikuwa akielezea umuhimu wa uuzaji wa wachezaji wachanga wa Ghana na kupata udhamini wakati akielezea kuwa Liverpool italipa zaidi ya euro milioni moja kwa kijana huyo.

Aliwaambia waandishi wa habari: “Nilipoanza mazungumzo ya uhamisho wa Abdul Issahaku Fatawu nje ya nchi, ilianza kutoka zaidi ya milioni moja na hii inamaanisha ikiwa tutapata udhamini wa kampuni, tunaweza kufanya vizuri zaidi”.
Issahaku, aliripotiwa kuigharimu Liverpool karibu pauni milioni 1.5, ambaye ameonyesha sifa yake inayokua nchini mwake, kama sehemu ya kikosi cha wakubwa cha Ghana.
Yoso huyo alikuwa mbadala asiyetumiwa katika pambano la kirafiki na Morocco na Ivory Coast mwezi huu, akiwa tayari amefunga goli katika kipigo cha timu ya ‘B’ dhidi ya Uzbekistan mnamo Machi.

Alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 20 mapema mwaka, baada ya kufunga mara mbili pamoja na moja kutoka ndani ya jitihada binafsi.
Hakuna uthibitisho rasmi wa uhamisho wa Fatawu Issahaku katika hatua hii, ingawa kutokana na hali ya makubaliano hayo kuna uwezekano kwamba ataelezewa na Liverpool.
Sporting CP inaweza kutangaza kuwasili kwake wakati mkopo utakapofanywa rasmi, venginevyo kuelekea kwake Merseyside kunaweza kuja na usajili wake, ambao unaweza kuwa mwishoni mwa 2021 wakati akitimiza umri wa miaka 18.(Goal).