ZASPOTI
MSHAMBULIAJI, Romelu Lukaku, amekataa kurejea kwenye Ligi Kuu ya England, lakini, ametajwa kumrithi, Robert Lewandowski huko Bayern Munich.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa mmoja wa wachezaji mashuhuri Ulaya tangu alipohamia Inter Milan.
Kabla ya hapo alifurahia mafanikio katika kiwango cha juu akiwa England akikipiga na Everton na kisha Manchester United.

Ilikuwa ni Chelsea ingawa ndiyo ya kwanza walimnunua kwenye Ligi Kuu ya England, lakini, ukosefu wa nafasi ulimlazimisha Lukaku, kuhama.
‘Blues’ wamehusishwa na uhamisho wa pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amefunga mara 64 katika misimu miwili iliyopita.
Alipoulizwa juu ya kurudi England, Lukaku, alidai ‘hafikirii’ uhamisho utafanyika na kusisitiza kujitolea kwake kwa Inter.

Mabingwa hao wa Italia wapo kwenye matatizo ya kifedha na wanaweza kulazimika kuwauza kwa fedha taslimu nyota wao wa hali ya juu.
Kocha, Antonio Conte tayari ameachana na klabu hiyo na raia mwenzake, Lukaku Emile Mpenza anaamini atakuwa sawa ikiwa atahamia Ujerumani kukipiga na Bayern.
Miamba hiyo ya ‘Bavarians’ wamefaidika kwa kuwa na mshambuliaji wao raia wa Poland, Robert Lewandowski, katika mfumo wa maisha yake kwa misimu miwili iliyopita na Lukaku ameungwa mkono kufanikiwa kwenye Bundesliga.

“Nguvu ya Romelu kwenye kupambana na kasi yake ni bora. Hiyo inafanya kuwa ngumu kwa mabeki dhidi yake”, alieleza, Mpenza.(Sport Bild).