DAKAR

NYOTA wa Liverpool, Sadio Mane, ametoa msaada wa pauni 500,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hospitali katika mji wa nyumbani kwao wa Bambali nchini Senegal.  Kijiji hicho hakijawahi kuwa na kituo kama hicho cha matibabu hapo awali.

Ukweli Mane anajua vizuri hali hiyo, kwani baba yake alikufa wakati alipokuwa na umri wa miaka saba baada ya hatoweza kufikishwa hospitalini kwa wakati kutibiwa maumivu ya tumbo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 tayari ameshatoa pauni 250,000 kujenga skuli huko Bambali.

Sasa ameongeza mara mbili kiasi hicho fedha kusaidia kujenga hospitali, akikutana na rais wa Senegal, Macky Sall, kutoa zawadi hiyo rasmi kwa serikali.
Hospitali hiyo itakuwa na idara ya A&E, utunzaji afya wa akinamama, vifaa vya meno na vyumba vya ushauri.

Mane hapo awali alizungumza juu ya kifo cha baba yake karibu na kutolewa kwa filamu, iliyotengezwa nchini Senegal juu ya maisha yake.
“Aliumwa na tumbo, lakini kwa sababu hakukuwa na hospitali, tulijaribu dawa za kienyeji,” alisema, Mane.

“Walimpeleka kijijini na alikufa huko. Kulikuwa na waasi wengi wakati huo, kwa hivyo hakukuwa na njia ya kumrudisha nyumbani. Walichagua kumzika huko.”
Ni aina hii ya janga ambalo hospitali Mane amefadhili na kuipa serikali kwa matumaini itaweza kulizuia.

Mane alikulia katika kijiji kidogo cha kilimo, akicheza mpira wa miguu kwa kutumia maboksi au matunda ya zabibu wakati hakukuwa na mipira iliyopatikana. Ni kijiji cha mbali na mji kama mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Matarajio ya kijana Mane kuwa mchezaji wa mpira wa miguu yalizingatiwa kama ndoto ya kushangaza, anaeleza.

“Watu waliniona sio wa kawaida,” alisema, Mane, mwaka jana. “Nilipomwambia mama yangu:” Nataka kuwa mwanasoka “, alidhani nilikuwa mwendawazimu. Kwake ilikuwa ndoto ya kitoto”.(AFP).