LONDON, England

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, yupo tayari kumtema Mshambuliaji, Anthony Martial, kwa sababu ya kuchanganyikiwa juu ya ujasiri na kiwango chake.
Ujasiri wa mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa umeelezewa kama ‘mbaya’ huku taarifa zikielezea uwezekano wa kuondoka majira ya joto.

Martial ameshuhudia msimu mgumu wa 2020/21, akifunga magoli saba tu katika michezo 36 kwenye michuano yote.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amepoteza nafasi yake kama mshambuliaji chaguo la kwanza wa United mbele ya Edinson Cavani, ambaye kuongezewa mkataba kunaacha hatma yake ya baadaye shakani.

Solskjaer anaripotiwa kupendelea kusaini mbadala wa muda mrefu wa Cavani pia ameashiria kuwa wakati wa Martial huko Old Trafford unakaribia kumalizika.
Kocha huyo inaelezwa amechoshwa na tabia ya Martial na kiwango kibovu huku akihusishwa na kutimkia Real Madrid.

“Martial atatolewa kafara iwapo watapata mshambuliaji mpya”, alisema.
“Solskjaer amechoka na tabia yake na hajavutiwa na utengenezaji wa magoli yake na kuunganishwa kwa kawaida kwenye timu msimu huu.”
Huenda pia Martial akatolewa Real Madrid kwa ada ya mkopo wa msimu mzima na chaguo la kumnunua msimu huu wa joto.

Ujio wa winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, unaweza kupunguza muda wa mchezo wa Martial wenyewe msimu ujao.
Pamoja na Cavani, Paul Pogba, Marcus Rashford na Mason Greenwood wote wanaonekana kuwa mbele katika safu ya kushambulia, Sancho atafanya matumaini yake ya dakika kuwa wazi.

Kukosekana kwa Martial kwenye Euro 2020 kwa sababu ya maumivu kunaweza kusababisha harakati juu ya uwezekano kuondoka United katika wiki zijazo.
Martial alisaini kandarasi mpya na United itakayombakisha Old Trafford mpaka Juni 2024.
Mshambuliaji huyo alijiunga na United akitokea Monaco mnamo Septemba 2015 kwa ada ya pauni milioni 36, lakini, hakuwa na furaha chini ya Jose Mourinho.

Chini ya Solskjaer akiwa kocha wa mpito, alimtaja Martial kuwa na ubongo mzuri wa mpira, ambao ukijumuishwa na kipaji chake cha kipekee kinamfanya awe mchezaji mwenye mustakabali mzuri.

Lakini sasa hali inaonekana kuwa kinyume na Solskjaer anamuangalia kivyengine Mfaransa huyo na yupo tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo.(Mirror).