WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema ina mpango wa kufanya mapitio ya mtaala wa msingi na maandalizi, ili kupunguza idadi ya masomo kwa elimu hiyo na kuifanya lugha ya kiengereza kuendelea kufundishwa kama somo kuanzia darasa la kwanza.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohamed Said, alieleza hayo wakati akimjibu suala la msingi Mwakilishi wa jimbo la Nungwi, Abdallah Abasi Wadi, alietaka kujua wizara haioni umuhimu wa kupunguza masomo katika skuli za msingi ili kulijengea umuhimu somo la kiengereza.

Alisema mabadiliko hayo yataimarisha lugha ya kiengereza na kuonekana  ina umuhimu wa pekee hasa katika mawasiliano ya kimataifa.

“Lugha ya kiengereza ina umuhimu katika mawasiliano ya mwanadamu kama ilivyo lugha ya kiswahili, Kiarabu, Kitaliana na Kifaransa”, alisema Waziri huyo.