NA MWAJUMA JUMA

KITENDAWILI cha timu moja itakayoungana na Hard Rock kushuka daraja msimu huu wa ligi 2020/2021 kitatenguliwa kesho Juni 11.

Ligi hiyo ambayo inafikia tamati itachezwa mechi tano zote kwa wakati mmoja ili kuepuka upangaji wa matokeo.

Katika michezo hiyo timu tano moja kati ya hizo itaungana na Hard Rock ambayo tayari imeshuka.

Timu hizo ni Black Sailor, Kipanga, Mlandege ambazo kila mmoja ina pointi 25, Chuoni na Polisi wana pointi 24.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo mabingwa hao watashuka katika dimba la Amaan kucheza na Black Sailor, wakati Chuoni na JKU watacheza katika uwanja wa Ngome Fuoni, huku Mafunzo na Kipanga wakicheza katika uwanja wa Mao Zedong A.

Michezo mengine itachezwa katika uwanja wa Mchangani kati ya Polisi na KVZ na Malindi na Mlandege watapambana katika uwanja wa Kinyasini.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi hiyo KMKM 41, Zimamoto 35, KVZ 34, Mafunzo 33, Malindi 29, JKU 27, Black SAILOR 25, Mlandege 25, Chuoni 24, Kipanga 24, Polisi 24 na Hard Rock 19.