TEL AVIV, ISRAEL

WAZIRI mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewatolea wito wabunge waipinge serikali mpya ya mseto itakayoongozwa na Naftali Bennett.

Netanyahu amemkosoa mrithi wake mtarajiwa akiandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba Bennett ameliuza eneo la Negev kwa chama cha waarabu cha Ra’am, ambacho kitajiunga na serikali ya mseto kwa mara ya kwanza, pamoja na jangwa la Negev kusini mwa Israel.

Inaripotiwa serikali ya mseto inajumuisha kipengele kinachositisha uvunjaji wa majengo yaliyojengwa kwa njia isiyo halali katika jangwa hilo, hali inayovitia wasiwasi vijiji vya Bedouin.