NA MWANDISHI WETU, OMKR

MJUMBE wa Kamati Kuu ya chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amewaahidi viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa ataendelea kuitumikia nchi pamoja na chama ili kuhakikisha dhamira yao inafikiwa.

Othman aliyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu ya ACT Wazalendo kilichofanyika katika  ukumbi wa hoteli ya Lamada  iliyopo Ilala Boma, jijini Dar es Salaam, baada ya kutambulishwa kwa wajumbe wa Kamati hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuhudhuria vikao vya kmati toka ateuliwe kushika wadhfa huo kuchukua nafasi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia Februari 17, mwaka huu.

Alisema imani aliyoipata kwa viongozi na wanachama katika kusimamia dhamira ya chama hicho, ndio njia pekee itakayomsaidia katika utendaji imara wa kufikia safari yao.

Alisisitiza kuwa bado kuna nafasi kubwa kwa viongozi wa chama hicho kuendelea kumuongoza katika utendaji wa kazi za kukiendeleza chama ili kuona mabadiliko katika taifa  yanapatikana.

Aidha aliwakumbusha wajumbe wa mkutano huo haja ya kuendeleza umoja na mshikamano ndani nan je ya chama kuendeleza mema yaliyoachwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Marehemu Maalim Seif sheriff Hamad.

Katika kikao hicho  ambacho ni cha kawaida kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, wajumbe 51 kutoka Tanzania bara na Zanzibar ni cha kwanza katika mwaka 2021, pamoja na mambo mengine kijadili hali ya siasa na maendeleo ya chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani, baada ya kikao hicho ilieleza kuwa pamoja na mambo mengimne kikao hicho kimeadhimia kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho kufuatia kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa hiyo ilieleza pia kikao hicho kilipitia ushiriki wa chama hicho katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa umoja wa kitaifa na kuwaongeza viongozi wa chama hicho kwa ushirikiano wanaoutoa kwa viongozi wengine wa serikali na kupongeza utendaji wa Rais dk. Hussein ali mwinyi na rais samia suluhu Hassan

Vile vile kikao hicho kiliazimia kuendelea kwa harakati za kisisa kwa njia ya mani ikiwa ni pamoja na kuchochea upatikanaji wa katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na sheria ya vyama vya siasa.