NA JOSEPH NGILISHO ARUSHA

SERIKALI imefungua milango kwa wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo kutoka nchi za Ulaya kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo cha alizeti, ufuta na mbogamboga.

baada ya kuwahakikishia uwepo wa Ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo na Kuanzisha kiwanda Cha kuchakata mazao.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Waziri wa kilimo na mifugo, Prof. Aldof Mkenda, wakati wa mkutano na wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo kutoka nchi za Ulaya  ulioandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Ulaya (EUBG) nchini Tanzania.

Alisema wawekezaji hao watapunguza changamoto ya mafuta ya kula pamoja na uzalishaji wa mbegu, kilimo cha matunda na mbogamboga hapa nchini ili waje kuwekeza na kuwasaidia wakulima wetu kupata soko la mazao hayo hapa nchini.

“Bei ya mafuta imepanda hivyo ni fursa kwa wakulima kuzalisha mazao ya mbegu za mafuta kwa wingi,” alieleza Mkenda.

Aidha Prof. Mkenda aliwaalika pia wawekezaji hao kuwekeza uzalishaji wa mbolea na viwatirifu kwani Tanzania inauhitaji wa mbolea takribani tani 700,000 kila mwaka  .

Wakati huo huo Prof. Mkenda akizungumzia suala la kupanda bei ya sukari nchini, alisema kuwa hakuna uhaba wa sukari kwa sababu serikali imeagiza tani 50,000 kutoka nje ya nchi huku viwanda vya ndani vikiendelea kuzalisha hivyo sukari itapungua Bei.

Baadhi ya wawekezaji hao, Rory Nightingale anayezalisha mazao ya mboga mboga hapa nchini pamoja na kuchakata matunda ya nanasi alisema hatua ya serikali kupunguza ushuru wa mazao ya mboga mboga kutawasaidia wawekezaji kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la TAHA, Jaquiline Mkindi, hatua ya serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji wa sekta ya kilimo kutaongeza uwekezaji na hivyo kuleta manufaa kwa wakulima kuweza kuuzwa mazao yao hapa nchini.

Aidha Mkindi aliiomba serikali kuendelea kuilinda ardhi yetu kupitia sheria zilizopo na kuweza kuwa na maeneo maalumu ya uwekezaji wa kilimo.